Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kimataifa  »  Wapania kuwapunguzia mateso walimbwende.
 »  Home  »  Nthelezi Nesaa  »  Wapania kuwapunguzia mateso walimbwende.
Wapania kuwapunguzia mateso walimbwende.
By Nthelezi Nesaa | Published  09/21/2006 | Habari za Kimataifa , Nthelezi Nesaa | Unrated
Na Mwanahabari wa HabariTanzania.com

Hivi karibuni mameya wa majiji ya Madrid nchini Hispania na Milano nchini Italia wamepania kuangalia upya suala zima la ushiriki na viwango katika mashindano ya mitindo na mavazi kwenye majiji yao.

Kwa taarifa zilizovifikia vyombo vya habari ni kwamba kuanzia sasa kutakuwa na viwango maalumu kuhusu umbo na uzito wa washiriki kulingana na takwimu kutoka nchi husika.

Hii imefikiwa baada ya kufahamika kuwa wasichana wengi wanaoshiriki urembo au maonyesho ya mavazi wanaishi maisha ya mateso ya kujikondesha ili kukidhi viwango vinavyotakiwa na waandaji wa mashindano hayo.

Katika dhana iliyojulikana kama wearing thin, wanaopinga ukimbau mbau huu wamesema kuwa wahusika wanateseka bila sababu na hili ni uvunjaji wa haki za binadamu.

Dina Memerenko toka Urusi alikiri kuwa hata wahusika wanahisi hivyo ila kwa vile hawana la kufanya bali wanahitaji pesa, hujikuta wakikabiliana na hayo mateso ili wapate pesa.

Alitoa mfano wa rafiki yake ambaye hakumtaja jina kuwa alikuwa akiishi kwa kula apple moja kila siku kwa siku tatu kabla ya kupanda jukwaani.

Meya wa Milano ambao husifika kama mji mkuu wa urembo na mitindo amebainisha wazi kuwa mifupa au ukondefu au ukimbau mbau huumiza mwili na akili. Hivyo ni mateso sawa na mateso mengine lazima yapigwe vita na kukomeshwa.

Kwa wafuatiliaji wasiopenda mifupa inayoonyeshwa mara nyingi kwenye majukwaa ya huko nyumbani, watapata lau pumzi maana hadi hili linatokea,nchi hasa za kiafrika zilikuwa zinafuata mkumbo tu bila kujali haiba inayovutia ya jamii ya kiafrika.

Kwa kuliona hili tunaamini binti zetu watapata nao ahueni kutokana na mateso na utumwa wa urembo na mitindo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.