Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  SHIDEPHA+ waaswa kushirikiana na waandishi
SHIDEPHA+ waaswa kushirikiana na waandishi
By Habari Tanzania | Published  09/18/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Priscar Ngonyani, Sumbawanga

WAATHIRIKA wa ugonjwa wa UKIMWI mkoani Rukwa, wametakiwa kufanya shughuli zao kwa kushirikisha vyombo vya habari ili waweze kusonga mbele kimaendeleo.

Hayo yamesemwa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Waathirika wa UKIMWI (SHIDEPHA+), mkoani Rukwa, Godfrey Mwikala katika uchaguzi wa chama hicho ngazi ya wilaya iliyohusisha Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Sumbawanga.

Mwikala alisema: “Waathirika wenzangu najivua leo madaraka ya uwenyekiti kwa chama hiki, lakini napenda kuwaambia kuwa tumieni vyombo vya habari kwa kila mtakachokifanya, msiwaogope waandishi, hawa ni chombo muhimu sana katika shughuli zenu.”

Alisema SHIDEPHA+ mkoani Rukwa, bila vyombo vya habari isingejulikana mahala popote pale, lakini kwa sasa chama hicho kinajulikana nchi nzima kupitia vyombo vya habari.

Katika uchaguzi huo wa SHIDEPHA+ ngazi ya wilaya uliosimamiwa na Ozem Chapita, Salum Korongo alichaguliwa kuwa mwenyekiti kwa kupata kura zote 25 baada ya wagombea wawili kujitoa. Waliojitoa ni Winnie Kayanza na Rose Ngao


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.