Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Arusha waomba ongezeko la bei ya vyakula lidhibitiwe
Arusha waomba ongezeko la bei ya vyakula lidhibitiwe
By Habari Tanzania | Published  05/24/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
WAKAZI wa Arusha, wameiomba serikali kuingilia kati ongezeko la mara kwa mara la bidhaa za vyakula kwenye maduka, ambazo zinapanda kila siku mjini hapa.
 
Uchunguzi uliofanywa jana na juzi, na mwandishi wa habari hii umebaini kuwa, sukari, mchele, maharage na unga wa mahindi umepanda kwa kiasi kikubwa katika maduka mjini hapa.
 
Imebainika kuwa kilo moja ya sukari iliyokuwa ikiuzwa kati ya 700 na 850, sasa hivi ni sh. 1,100 hadi 1,300.
 
Wakati mchele kwa sasa unauzwa kilo moja 1200, wakati awali ulikuwa ukiuzwa shilingi 700 na 800. Pia imebainika kilo moja ya maharage ilikuwa ikuzwa sh. 700 ambapo kwa bei ya sasa ni sh. 800 na 850, kutegemeana na sehemu unaponunulia.
 
Wakati unga wa mahindi kwa bei kawaida kwa kilo moja ilikuwa 500 na 550 na sasa ni sh. 600 hadi 700, kutegemeana duka unalo nunulia.
 
Victor Robert wa M&M, wa makao mapya jijini hapa alisema kuwa maisha yamekuwa juu sana na kwamba wananchi wa kawaida watashindwa kupata mahitaji hayo muhimu, kutokana na kupanda kwa gharama hizo mara kwa mara.
 
Naye Khadija Musa wa Majengo alisema kuwa wanaiomba serikali kuingilia kati mfumuko huo holela wa bei mkoani hapa, kwa kuwa wanaoumia ni wanawake na watoto ambao wengi wanapata kipato cha chini.
 
"Angalia mwanaume anaacha sh. 1,000 asubuhi na akirudi jioni anataka kula ugali na nyama, ukimwambia hela haitoshi ni ugomvi mkubwa sana," alilalama Khadija.
 
Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la nishati ya mafuta ya taa, petroli na dizeli na kuleta mtafaruku mkubwa mjini hapa baada ya nauli za mabasi kupanda ghafla.
 
Wananchi wengine waliotoa maoni yao walisema kuwa kila kitu sasa hakishikiki na hivyo hawana pa kukimbilia zaidi ya kuiomba serikali kudhibiti ongezeko hilo holela la bei.
 
Baadhi ya wamiliki wa maduka waliozungumza na kuomba kutotajwa majina yao walisema ongezeko hilo linatokana na gharama za uzalishaji kupanda katika viwanda wanavyonunulia nafaka hizo.
 
Mbali na hilo pia walisema ongezeko hilo limetokana na gharama za usafiri, na kuiomba serikali kuingilia kati mfumuko wa bei za mafuta ili na wao wapunguze bei za bidhaa za vyakula madukani.
 
Kutoka gazeti la Uhuru
ISSN 0876-3896 NA.19318
Na Omari Shaaban, Arusha

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.