Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mbunge wa Kishapu adaiwa kutapeli
Mbunge wa Kishapu adaiwa kutapeli
By Habari Tanzania | Published  09/18/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Tullo Chambo

HALI ya mambo katika Jimbo la Kishapu, mkoani Shinyanga imechafuka.

Hali hiyo imetokea baada ya kuibuka kwa makundi mawili yanayopingana kuhusu tabia na mwenendo wa Mbunge wa jimbo hilo, Fred Mpendezoe Tungu.

Tayari mbunge huyo amekwisha kushitakiwa kwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, na kwa viongozi kadhaa wa CCM, na mmoja wa waliokuwa wasaidizi wake wa karibu katika masuala ya kifamilia na wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Taarifa zilizoifikia Tanzania Daima zinaeleza kuwa Mpendazoe anatuhumiwa na baadhi ya wasaidizi wake wa zamani walioshirikiana naye kwa karibu katika kampeni za Uchaguzi Mkuu kuwa amewadhulumu fedha za malipo yao kwa kazi walizomfanyia kwa nyakati tofauti.

Mmoja wa watu hao ameliambia gazeti hili kuwa, kwa nyakati tofauti alikubaliana na mbunge huyo kumfanyia kazi zake mbalimbali, ikiwamo kufuatilia uhamisho wa gari, matengenezo ya nyumba yake na kutafuta uhamisho wa shule wa watoto wake.

Alisema walikubaliana malipo ya kazi hizo kuwa ni sh 400,000, lakini baada ya kukamilisha kazi hizo kwa ufanisi, amekataa kumlipa.

Msaidizi huyo wa Mpendazoe aliyejitambulisha kwa jina la Anthony Sollo, alisema pamoja na kufanya kazi za Mpendazoe kwa uaminifu, zikiwamo za hatari ili kuhakikisha kuwa mambo yake yanakwenda sawa, ameshindwa kumlipa fedha zake na sasa anatoa vitisho kuwa atawashughulikia wote wanaomfuata fuata na kumchafua.

Sollo alisema amefuatilia malipo yake tangu mwaka 2004 bila mafanikio na baadhi ya wapambe wa Mpendazoe sasa wanamtishia kumuua iwapo ataendelea na madai hayo na kutoa siri za mbunge huyo.

Alisema yeye pamoja na wenzake wameamua kuungana ili kupambana na kundi la Mpendazoe na wataanza kwa kuanika madhambi yake aliyoyafanya wakati wa kampeni za mwaka jana.

Aliyataja baadhi ya madhambi hayo kuwa ni kununua gari la serikali kinyume cha taratibu na kuandika barua za kuomba ufadhili wa fedha kwa ajili ya wananchi wa Jimbo la Kishapu katika kampuni mbali mbali kwa kutumia nyadhifa za viongozi wa wilaya hiyo bila wao kuwa na taarifa.

Sollo alisema Mpendazoe alitumia njia za udanganyifu akiwa mfanyakazi wa Wizara ya Maji na Maendeleo ya Mifugo, kujipatia mamilioni ya fedha kutoka kwa wafadhili mbalimbali ambazo alizitumia katika kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Inadaiwa kwamba madhambi ya Mpendazeo yamekwisha kuripotiwa kwa Spika Samuel Sitta, Ofisi ya Bunge, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu, Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Taasisi ya Kuzuia Rushwa (PCB) na Polisi, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya mbunge huyo.

Hata hivyo vyanzo vingine vya habari vimeeleza kuwa Mpendazoe aliwahi kuonywa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Maendeleo ya Mifugo, Vincent Mrisho, baada ya kubainika kutaka kununua gari la serikali lenya namba STJ 5097 kinyume cha taratibu za ununuzi.

Njama za Mpendazoe kutaka kununua gari hilo kwa njia za panya ziligunduliwa na Kamati ya Fedha ya Bunge na ikaagiza apewe onyo kali, jambo ambalo lilifanywa na Mrisho.

Alipoulizwa kwa njia ya simu kutoka Kishapu, Mpendazoe alikiri kudaiwa na Sollo ambaye alieleza kuwa ni ndugu yake lakini alidai ni tapeli.

Alisema anamfahamu Sollo na amemsaidia mambo mengi hasa katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu lakini ameshindwa kumlipa fedha zake baada ya kuanza kumchafua kwa kutoa siri zake sehemu mbalimbali ambazo hakutegemea.

“Huyo bwana namjua ni ndugu yangu, ni kweli tulikuwa na makubaliano fulani ambayo mimi sijayatekeleza, lakini ameniudhi sana baada ya kuzunguka sehemu mbalimbali na kuanza kutoa siri zangu,” alisema.

“Kote alikokwenda wamempuuza, amefika hadi kwa Spika, NEC, PCB hadi Polisi ili kunichafua, lakini wamempuuza, sasa anatumia vitisho ili nimlipe, kwa nini?

“Wee ndugu yangu naomba uyaache hayo, nisubiri mwezi huu tarehe 26, nitakuja Dar es Salaam, tutazungumza vizuri, nitawapa ufafanuzi wote lakini huyo ni tapeli, amenunuliwa na wanasiasa ili anichafue, na nitaomba muwe mashahidi wangu” alisema Mpendazoe.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.