Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wizara ya Maliasili yamdhibiti Sauper
Wizara ya Maliasili yamdhibiti Sauper
By Habari Tanzania | Published  09/17/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

WIZARA ya Maliasili na Utalii, kwa kuwatumia wataalamu wake na wa intaneti, imefanikiwa kuingiza taarifa kwenye mtandao zikilenga kuikosoa filamu ya Darwin’s Nightmare.

Habari kutoka wizarani hapo zimesema kwamba, kutokana na ‘utundu’ huo, sasa kila anayefungua website yenye kuelezea filamu hiyo, lazima akutane na tamko la serikali kuhusu kile kinachoitwa upotoshaji uliofanywa na Hubert Sauper.

“Ukifungua google, yahoo, msn ukitafuta Darwin’s Nightmare, lazima pembeni utaona msimamo wa serikali unaotoa upande wa pili na ukweli kuhusu kile kilichopotoshwa kwenye filamu hiyo, na pia katika partner site million 21” alisema mmoja wa walioshiriki kufanikisha kazi hiyo.

Mtaalamu huyo alisema walipata msukumo wa kutekeleza wazo hilo, baada ya kushauriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Anthony Diallo, ambaye pia ni mtaalamu wa biashara za elektroniki zinazohusu intaneti.

“Tunatarajia kuwa wasomaji milioni 50 watakuwa wamesoma taarifa halisi ya serikali katika kipindi cha miezi miwili hadi mitatu.

“Hii ni web attack, ni vita ya elektroniki, lazima na sisi tuipigane ki-eletroniki ili tupate ushindi.

“Tukipigana kwa kukanusha tu kwenye vyombo vingine vya habari, tunaweza tusifanikiwe sana kama tukitumia njia hii tuliyoamua kuitumia.

“Sasa kila atakayetaka kuijua Darwin’s Nightmare, basi hapo hapo atapata upande wa pili, yaani tamko la serikali yetu, kwa hiyo msomaji atajua kuwa filamu hii iliandaliwa kutuchafua Watanzania na kuharibu kabisa biashara ya samaki wetu Ulaya,” alisema mtaalamu huyo.

Filamu hiyo iliandaliwa mwaka 2004. Inaonyesha biashara ya samaki Ulaya na ulaji mabaki ya sangara (mapanki) kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa.

Pia inazungumzia ukahaba na kuenea kwa UKIMWI; na usafirishaji silaha katika eneo la maziwa makuu.

Yote hayo yamekanushwa vikali na Rais Jakaya Kikwete. Lakini walioiona, wanakubaliana na mengi, isipokuwa usafirishaji silaha.

http://www.darwinsnightmare.net

Source: Tanzania Daima



How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.