Serikali inadai imempiga bao mwandishi na mtunzi wa documentary ya Darwin’s Nightmare. Kilichofanyika na ambacho walitakiwa wafanye hata kabla ya longolongo lililotinga hadi Bungeni ni kuweka taarifa kupinga yale yote yaliyorushwa na kuonyeshwa ndani ya filamu hiyo.
http://www.darwinsnightmare.net/
Kwa kusaka documentary hiyo ndani ya search engine ya google.com, link ya kwanza utakayopata ni tamko la serikali linaloelezea msimamo wake juu ya kila kilichoko ndani ya documentary hiyo iliyojadiliwa Bungeni na mikakati ya kukabiliana nayo kupangwa.
Filamu hiyo ya Hubert Sauper imeitikisa Bongo kwa kuihusisha na ulaji mapanki (si yaliyooza), biashara ya silaha, njaa, watoto wa mitaani na ukahaba uliokithiri unaofanyika katika jiji la Mwanza nchini Tanzania.
Hata hivyo maelezo ya Hubert Sauper yanadai kuwa alifanya hivyo ili kuisadia Bongo ijulikane zaidi na iweze kupatiwa misaada ya kukabiliana na hali hiyo.
Ili kupata tamko la serikali fungua link hii
http://www.darwinsnightmare.net/
SOURCE: DARHOTWIRE.COMhttp://www.darhotwire.com/dar/Biashara/2006/08/22/23099.html